Naibu waziri mkuu ambaye pia ni mbunge wa gatundu kaskazini uhuru kenyatta na balozi francis muthaura ambao wanakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya icc hatimaye wamejiuzulu kutoka nyadhifa zao serikalini. Ni hatua inayodhihirisha msema lisilobudi hutedwa, lakini kama anavyotuarifu mwanahabari frank otieno kenyatta amejiuzulu tu kama waziri wa fedha na wala sio naibu waziri katika serikali ya muungano.