Mwanafunzi mwingine aliyefanya mtihani wa kcpe mwaka uliopita amejitia kitanzi katika eneo la mumias kaunti ya kakamega. Wazazi wake sylvester atsango hata hivyo wamekanusha madai kwamba huenda ni kwa sababu ya alama alizopata au shule aliyoitwa kuendeleza masomo yake ya shule ya upili. Mwili wa sylvester anayedaiwa kuwa na hamu kuu ya kujiunga na shule ya upili ulipatikana ukining'inia kwenye kamba katika mlango wa kabati ndani ya chumba chake cha kulala.