Uchaguzi wa chama cha odm huko bungoma uligeuka na kuwa uwanja wa kurushiana makonde baada ya mjumbe mmoja kumzuilia waziri alfred sambu kutoka kwenye kituo cha kupigia kura. Na hapa jijini nairobi bodi ya uchaguzi ya chama cha odm imefutilia mbali uchaguzi wa kaunti ya nairobi na kutaka uchaguzi huo kurejelewa tena hapo kesho.mbunge wa starehe margret wanjiru alijiondoa kwenye uchaguzi wa leo baada ya tofauti kuibuka baina yake na mbunge wa zamani reuben ndolo.