Maandalizi ya mwisho yawatahiniwa wa kidato cha nne yanaendelea katika shule zote za upili nchini kabla kuanza kwa mtihani wa kitaifa wa KCSE siku ya jumanne. Shule kadhaa nchini leo zilifanya maombi maalum kwa watahiniwa hao 431,000 huku wizara ya elimu ikiapa kuyafutilia mbali matokeo ya mwanafunzi atakayepatikana akidanganya.. Hatahivyo baadhi ya wanafunzi wako taabani baada ya kusajiliwa kimakosa masomo ambayo hawakuwa wakiyaosma na kuibua swala kwa uwajibikaji wa tume simamizi ya KNEC