Mashirika mbali mbali ya humu nchini yakiwemo yale ya vyombo vya habari yamehusika katika sherehe maalum ya  kuchangisha fedha kupitia mpango wa kenyan for kenyans. Kwenye hafla ya leo iliyofana takriban  shilingi millioni 255  ziliweza kuchangwa na kufikia leo jioni hazina ya  kenyan for kenyans kufikia iliorodheshwa kuwa imefikisha shilingi zaidi ya shillingi millioni 480 . Huu ukiwa ni mfano mzuri kutoka kwa wakenya waliojitolea kuhakikisha kuwa wenzao kutoka maeneo kame  hawafi njaa kama ilivyoshuhudiwa mwezi uliopita.


Kenyans for Kenya fundraiser-Swahili