Wabunge hii leo wameibua tena suala la ajira kwa wafanyikazi katika mabaraza ya miji ikihofiwa kuwa huenda baadhi ya madiwani wakapoteza ajira pindi serikali za ugatuzi zitakapobuniwa.hili limechochewa na pendekezo la kupunguza idadi ya wadi zilizoko lakini waziri wa serikali za wilaya musalia mudavadi ametoa hakikisho kwamba ingawa baadhi ya wadi zitawekwa pamoja hakuna yeyote atakayepoteza ajira.mbali na hayo jopokazi linaloshughulikia serikali za ugatuzi limeahidi kufanya mkutano na wizara ya fedha ili kutafuta mwafaka kuhusiana na tofauti zinazozingira miswada tofauti ambayo wameikabidhi tume ya utekelezaji wa katiba kuhusiana na sheria zitakazodhibiti mgao wa fedha za umma.


Devolution conference