Huenda ongezeko la bei ya mafuta humu nchini likawa ni njama baina ya wanasiasa wachache wanaonuia kuchangisha pesa za kampeini za uchaguzi wa mwaka wa 2012 kwa  kuwafilisisha wakenya. Haya yaliibuka katika kikao cha bunge leo hii ambapo kamati ya bunge ya masuala ya kawi ilipowahoji wadau kutoka sekta hiyo. Vilevile inaonekana sio tu gharama ya kimataifa ya mafuta inayochangia ongezeko hili bali pia vita baina ya wadau wakuu wakiwemo wale kutoka sekta ya kibinafsi na serikali huku kila mmoja akimlaumu mwenzake. Carol nderi aliyehudhuria kikao hicho anatupasha zaidi.


2012;fuel;kiraitu;imanyara;