Zimesalia siku mbili pekee na raia wa taifa la  Uganda wanatarajia kufanya uchaguzi utakaomteua Rais wa nchi hio ambaye huenda akamtoa mamlakani Yoweri Kaguta Museveni ambaye ameshikilia wadhifa huo kwa muda wa miaka ishirini na tano. Kufikia sasa kampeini za uchaguzi zimefika  kikomo na wapinzani wakuu wa uchaguzi huo ni  Yoweri Museveni na Kiza Besigye ambao wametoa ahadi za kuimarisha uchumi wa taifa hilo pamoja na kuahidi kazi kwa vijana .


Kampeni Uganda