Serikali imetangaza kuwa hakuna mkenya atakayekosa chakula hata iwapo taifa linapitia kipindi kigumu cha baa la njaa, hii ni licha ya makali ya njaa kutokana na kiangazi katika sehemu kadhaa humu nchini kuzidi kuwaathiri wananchi na wengine kulazimika kula matunda ya mwitu huku baadhi ya watoto wakikosa kuhudhuria shule katika baadhi ya maeneo kutokana na njaa.  Frank Otieno anatufungulia taarifa zetu kwa kuangazia jinsi hali inavyozidi kuwa mbaya, huku kwengineko vyakula vya msaada vinavyopelekwa   katika baadhi ya sehemu hizo vimeripotiwa kutoweka katika hali ya kutatanisha.


Athari Za Ukame