Kuna hofu kuu miongoni mwa wakaazi wa jiji la Nairobi kwamba nyama wanayoila wakidhani ni ya ngombe huenda ni ya punda. Baada ya lalama za wenye punda kadhaa kwamba mifugo wao wanapotea wasijue wanakwenda wapi, sasa jawabu limeanza kujitokeza. Hii leo vichwa vya punda wanne vimepatikana katika eneo la mihang’o ishara kwamba wamechinjwa na nyama kupelekwa katika bucha kuuzwa kama nyama inayopaswa kuliwa na binadamu.Kiini cha hofu hapa ni kwamba ni kwa wiki jana tu ambapo kisa sawa na hicho kilishuhudiwa maeneo ya Kitengela.


Nyama Ya Punde Kayole