Aziri wa barabara Franklin Bett amesema mpango wa upanuzi wa barabara ya Mombasa sasa umesitishwa baada ya benki ya ulimwengu kujiondoa kutoka kwenye ufadhili wa barabara hiyo. Bett amesema sasa serikali italazimika kuanza upya mpango wa kutafuta wafadhili wapya ili kufanikisha mpango huo. Hatua hii imejiri huku mpango wa upanuzi wa barabara ya Mombasa ukizingirwa na utata huku baadhi ya wawekezaji wa kibinafsi katika barabara hiyo wakihofia kuwa huenda majengo yao yakabomolewa.


Upanuzi Wa Mombasa Road