Maisha ya aliyekuwa afisa mkuu wa polisi Mohammed Jarso Godana imo hatarini siku moja tu baada ya kupasua mbarika kuhusiana na wahusika katika sakata ya ulanguzi wa madawa ya kulevya mjini Mombasa. Mohammed Jarso Godana afisa chapa kazi aliachishwa kazi baada ya kuzuia konteina elfu tatu iliyokuwa ikibeba dawa za kulevya aina ya cocaine. Hapo jana afisa huyo alifanikiwa kuwasilisha cheti cha siri mkikononi mwa mbunge wa Imenti ya kati Gitobu Imanyara kulijadili bungeni inayowataja wahusika wakuu miongoni mwao maafisa wakuu wa usalama. Hata hivyo msemaji wa polisi Eric Kiraithe amepuuzilia mbali taarifa hizo na kuzitaja kama finyu na za kupotosha.