Huku vita dhidi ya ufisadi vikiendelea kupamba moto serikalini, kuna madai kwamba vita hivi vinachukua mwelekeo tofauti pamoja na kupata muingilio wa kisiasa.Kuna wanaodai kwamba baadhi ya wanasiasa wameanza kutumia vita dhidi ya ufisadi kama kigezo cha kujipatia umaarufu pale wanapowaumbua wenzao wanaodaiwa kuhusika na kashfa za ufisadi. Lakini kwa sasa kitendawili ambacho kinakosesha wengi usingizi ni kuambatana na hatua ya waziri mkuu kumtetea waziri wa maji Charity Ngilu dhidi ya tuhuma za ufisadi na hivyo kuibua suala jee ni yepi anayojua kuambatana na sakata hii?


Siasa Za Ufisadi