Zikisalia chache kabla ya wenyeji wa maeneo ya starehe, Juja na Makadara kuelekea debeni kwa chaguzi ndogo za maeneo hayo, mtazamaji hii leo tunapigia darubini eneo bunge la Juja ambalo linaonekana kukabiliwa na changamoto si haba kuambatana na maendeleo.ni eneo linalotambulika kwa rotuba yake na historia ya kuwa jiji la viwanda, lakini kinachoibuka ni kwamba baadhi ya viwanda vimesambaratika na hivyo kuacha wengi bila ajira.Jee tatizo limekuwa wapi?na jee wenyeji wanatafuta kiongozi wa aina gani?