Mgogoro kuambatana na majukumu ya utawala wa mikoa chini ya katiba mpya hii leo umechukua mkondo mpya huku mawaziri Noah Wekesa na Mutula Kilonzo wakitangaza kutofahamu lolote kuhusiana na maafikiano ya baraza la mawaziri kuhusu suala hili.hayo yakiarifiwa afisi ya rais imedaiwa kutuma wawakilishi kutoka utawala wa mikoa nchini Brazil kujipa ufahamu kuhusiana na majukumu ya utawala wa mikoa chini ya mfumo wa ugatuzi nchini humo.