Rais Mwai Kibaki hii leo aliongoza kampeni za ndio mkoani mashariki ambako alihimiza wenyeji kukumbatia katiba inayopendekezwa.akizungumza katika eneo la Kitui, rais alisisitiza kuwa katiba inayopendekezwa imejaribu kushughulikia masuala ambayo hayakuweza kutimizwa kupitia katiba ya Lancaster na kusisitiza kuwa hoja zilizosalia zitashughulikiwa baadaye.Kampeni hizi ambazo zimefikia kikomo hii leo pia zilielekezwa hadi katika eneo la Kiambu.