Kwa miaka na mikaka viongozi nchini wamekuwa wakiongoza taifa hili katika misingi ya kikabila kando na kuiteka nyara idara nzima ya usalama kwa lengo la kujinufaisha wao wenyewe. Si jambo geni kuona mtu fulani akipewa cheo pasi na kuhitimu eti kwa sababu yeye anatoka katika jamii ya kiongozi huyo. Je, ni lini tabia hii itadidimia, je katiba mpya itageuza hali hii. kwa mengi zaidi huyu hapa Mohammed Ali na taarifa yake kuhusu usalama wa taifa katika msururu wetu wa makala ya katiba.