Baadhi ya viongozi kutoka mkoa wa Rift Valley wamepinga vikali hatua ya waziri wa fedha Uhuru Kenyatta, kupunguza ada ya kuagiza ngano na bidhaa zake kutoka nchi za nje, hatua iliyopelekea wakulima wangano nchini kufanya maandamano kulalamikia bei duni ya ngano nchini, hali wanayodai imewasababishia hasara tupu.