Dhana kuu inayoaminika na wengi ni kuwa wingi wa mvua humaanisha wingi wa mavuno mashambani na hivi wengi hutarajia kuwa vyakula vitauzwa kwa bei nafuu. lakini la kushangaza ni kuwa yanayotendeka wakati huu wa mvua ni kinyume na matarajio ya wengi. Sanduku moja la nyanya kwa sasa linauzwa kwa shilingi elfu saba kinyume na bei ya kawaida ya shilingi elfu mbili au hata elfu tatu. Mwanahabari wetu Carol Nderi alizuru baadhi ya maeneo ya mauzo na kutuandalia taarifa ifuatayo.