Huenda shughuli ya kuelimisha umma kuhusu rasimu isiendeshwe ipasavyo baada ya kamati ya wataalam kukosa fedha za kufadhili shughuli hiyo. Kufikia sasa kamati hiyo imepokea shllingi millioni 10 pekee tofauti na ilivyotarajiwa kwamba wangelipata shillingi millioni 330 kutoka kwa wizara ya fedha. ni hali ambayo imemshurutisha kamati hiyo kutoa ombi maalum kwa waziri Uhuru Kenyatta kuingilia kati kutatua vikwazo vinavyochelewesha harakati hii.