Huku hatua ya kupanda kwa uzalishaji wa maziwa nchini ikizidi kutatiza wakulima wanaolazimika kuyamwaga maziwa yao kutokana na kampuni za maziwa kutoweza kumudu kiwango hicho cha maziwa, maswali yanayoibuka ni je,mbona serikali inashindwa kumudu hali hii ilhali ina uwezo wa kuyahifadhi maziwa hayo. Wataalam wa sera za kilimo wanasema serikali inafaa kubuni sera nzuri na mipango thabiti ya kukabiliana na mazao mengi hasa baada ya mvua nyingi kushuhudiwa.


Milk Oversupply; kcc;