Wizara ya nyumba itajenga vituo vya kuhamasisha umma kuhusu kanuni za ujenzi pamoja na umuhimu wa ujenzi bora kote nchini ili kuchangia katika kuongeza nyumba zilizo salama kwa raia. Akizindua kituo kimoja kama hicho cha kuhamasisha umma huko mukurwe –ini waziri msaidizi wa makao Margaret Wanjiru alidokeza kuwa vituo hivyo pia vitachangia katika kupunguza gharama ya ujenzi.