Huku tukiadhimisha Siku ya Ukimwi Kote Ulimwengu, humu nchini takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya maambukizi kati ya watu wenye umri wa miaka 15 hadi 60 imeongezeka.

Akihutubia umma, Waziri wa Mipango Maalum Naomi Shaban amedokeza kuwa serikali itahakikisha kuwa maambukizi ya virusi vya ukimwi yanapungua kote nchini.