Huku siku zikichongea kumalizika kwa tarehe ya wananchi wa kenya kujiandikisha kuwa wapiga kura, uhamasisho wa wakaazi kutoka eneo bunge la Emuhaya kaunti ya Vihiga kujitoa kimaso maso kukata kura unazidi kuendelezwa kila kona za sehemu hiyo chini ya askofu wa kanisa la Upendo Pentecostal Fellowship nchini askofu charles sande na kuwaeleza kinaga ubaga umuhimu wa kupiga kura ili kubadilisha uongozi mahususi katika taifa hili.
Akizungumza kwenye hafla ya uhamasisho huo maeneo mbalimbali wilayani emuhaya, askofu sande amedokeza kuwa, swala la kuchukua kura na kupiga lipo hata kwenye bibilia ambapo linafaa kutiliwa maanani zaidi na kuwekewa uzito wa aina yake kwa lengo la kunusuru uchumi wa wananchi wa kenya.
READ MORE
Why William Ruto has every reason to panic
The ritual of voting amid the crisis of belief among voters
When systems are not trusted, agency finds another path
We must give voter registration numbers same dignity as taxes