Mwanamume mmoja amekiri mashtaka ya kushiriki ngono katika Bustani ya Uhuru, jijini Nairobi wakati wa mchana.
Mwanamume huyo kwa jina Kanara Maina amefikishwa mbele ya Hakimu, Joseline Onga'yo ambapo ametozwa faini ya shilingi 1,500 ama ahudumu kifungo cha mwezi mmoja jela.
Maina amekiri kutekeleza kitendo hicho na mwanamke kwa jina Joyce Wanjiku. Licha ya kuomba msamaha, hakimu Ong'ayo amemtoza faini hiyo akisema kitendo hicho ni kinyume na sheria za Jiji la Nairobi ambazo haziruhusu vitendo vya aina hiyo katika maeneo ya umma.
Wanjiku hata hivyo hakujiwasilisha mahakamani baada ya kuachiliwa kwa dhamana wiki iliyopita walipokamatwa.