Wakulima wanatarajiwa kunufaika kwa kununua mbolea kwa bei nafuu katika Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao, NCPB.

Hatua hii inajiri baada ya serikali kutoka shilingi bilioni 3.5 kuwa ruzuku ya Mbolea

Katibu wa Wizara ya Kilimo Francis Owino amesema mbolea kilo 50 ya aina ya DAP itauzwa kwa shilingi 3, 500, CAN shilingi 2,875, UREA 3,500, NPK 3275, MOP 1,775 na Sulphate of Ammonia shilingi 2,220.

Katibu Owino ametoa hakikisho kwa Wakulima kwamba tayari mbolea hiyo imewasilishwa katika ofisi za NCPB kote nchini jinsi alivyoagiza Rais William Ruto.

Hata ivyo, wakulima wanaruhusiwa kununua mbolea hadi magunia mia moja ya kilo 50.

Ikumbukwe Rais Ruto aliagiza kupunguzwa kwa bei za mbolea kutoka shilingi 6,500 kwa kila kilo 50, wakati wa kuapishwa Jumanne iliyopita.


NCPB William Ruto Francis Owino