Shule za kutwa katika Kaunti ya Kakamega, Mombasa na maeneo bunge ya Rongai, Kacheliba, Kitui Rural na Pokot Kusini zitafungwa kwa siku moja, tarehe 29 wiki ijayo kupisha uchaguzi.
Kwa mujibu wa Waziri wa Elimu Prof. George Magoha, shule za mabweni hazitafungwa wala kuathirika kutokana na uchaguzi huo.
Jumatatu, IEBC iliafikiana na wawaniaji wa viti mbambali kuyoka maeneo ambako uchaguzi haukufanyika tarehe 9 mwezi Agosti, kwamba ufanyike Jumatatu wiki ijayo.
Ikumbukwe, vituo vingi vya kupigia kura huwa katika shule za umma.