Na, Suleiman Yeri Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao, NCPB imefichua kwamba itawasilisha majina ya watu themanini kwa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC kuchunguzwa kwa wizi wa mbolea iliyopunguzwa bei. Mwenyekiti wa NCPB, Geoffrey King'ang'i amesema polisi wanawachunguza baadhi ya watu wanaoshukiwa kupakia upya mbolea hiyo na kuwauzia kwa bei ya juu watu wasiostahili. Bodi hiyo aidha imekiri kwamba wafanyakazi wake arubaini na watatu walishirikiana na maafisa wa kilimo na maafisa wa utawala kuiba mbolea hiyo iliyofaa kuuziwa wakulima kuboresha mazao yao kwa bei nafuu. King'ang'i, amesema takribani maafisa ishirini na wawili wa ngazi ya juu waliosimamishwa kazi na katibu katika Wizara ya Kilimo, Richard Lesiyampe ni miongoni mwa watu wanaochunguzwa