K
una watu wengine wamejiwekelea tabia ya kudharau wengine sana.
Yani unadharau mwenzako yet siku hizi kila mtu ni shatah kivyake. Hauwezi ukadharau mtu kwa kumuangalia na hamujawahi kutana na yeye. Imagine hamjawahi bonga na hamjuani na huyo mtu but unamuonyesha madharau.
Madharau sio poa sana kwa mtu usiyemjua. Unaweza ukadharau mtu kumbe yeye ndiye sonko wako wa future. Unapata unaenda kusakanya works unakuta mwenye ulidharau ndie ako kwa offy kama sonko. Then unaanza kuaibika juu tu ya madharau.
Ukimdharau ulikua shatah, sasa yeye ndie shata, na anaweza akakudharau. Ndio nataka kila mtu akae akijua kila mtu ni shatah kivyake, na huwezi ukatoa ushata yake kwake.
Wamama wa mboga wasidharauliwe. Hao ni mashatah kivyao juu bila wao nani angekua ameturahisishia job ya kukatakata mboga. Watu hawa wamesaidia sana mabachelor na masingles. Na si hao tu, hata mabibi wenye wameolewa wengi wao hawajui kukatakata sukuma juu ya mama wa mboga.
Wife zake ni kupika tu sembe kwa keja halafu anakimbilia sukuma kwa kibanda yenye mboga imekatakatwa kama machine. Hawa wamama wa mboga ni mashatah, mathree, taxi, tuktuk na manduthi, madere na madonda hata kama hawafuatangi sheria za barabara venye inafaa. Hao wasee ni mashatah kivyao. Tunawahitaji kwa njia moja ama nyingine.
Pia wewe mwenyewe ni lazima ujiheshimu kwa sababu wewe ni shatah kivyako. Bila wewe, Kenya tungekua less na mtu mmoja. But wewe ni shatah kwa kua mkenya unajilisha, unajilipia bills, uanasomesha watoto wako wapate elimu. Wewe ni shatah, wewe ni shatah mpaka unasaidia serikali ki uchumi. Bila wewe serikali ingekua inakata nani tax? Na ndio maana nasema kila mtu ni shatah kivyake tusare kudharauliana.