Na Fredrick Muitiriri
NAIROBI, KENYA, HATIMAYE mwandishi wa hotuba iliyosomwa na mkewe mgombea urais nchini Marekani Donald Trump, Melania Trump, ameomba msamaha kwa kuandika hotuba hiyo bila kuzingatia sheria za uandishi.
Meredith Melver amemwomba mkewe Rais wa Marekani Michelle Obama msamaha kwa kughushi hotuba yake aliyoitoa mwaka wa 2008 kabla ya Rais Barrack Obama kuwa Rais.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Meredith amesema mkewe Trump alimweleza kuwa anamwenzi sana Michelle Obama ndiyo maana akadondoa baadhi ya sehemu za hotuba hiyo ya mwaka 2008 ambayo alisema humpa motisha.
Aidha, ameeleza kuwa aliitumia bila kukagua hotuba hiyo ya Michelle na kufanya kosa hilo la kuitumia moja kwa moja.
Vilevile, amewaomba Wamarekani msamaha.