Kufuatia mauaji ya siku ya krismasi mjini isiolo afisa mkuu wa utawala eneo hilo isaiah mburu alifanya mkutano wa amani na wazee wa jamii, za waturkana, wasomalia na waborana mchana wa leo katika makao makuu ya wilaya ya isiolo. Kwenye mkutano huo, wazee kutoka jamii zinazozana, walilaumiana kuhusiana na tukio la hapo juzi. Si mara moja au mbili eneo la isiolo limewazika waathiriwa wa mashambulizi kati ya jamii hizi, tatizo likiwa ardhi, lishe, maji na hata siasa. Ali manzu anaarifu zaidi.