Wiki jana ulimwengu uliadhimisha siku ya kisukari,ugonjwa unaotambulika kunyemelea watu kutoka tabaka mbalimbali matajiri na maskini kwa pamoja. Ni ugonjwa unaoweza kudhibitiwa na hata kuzuiliwa iwapo unakuwa mwangalifu katika lishe na mazoezi ya kila mara. Uognjwa wa kisukari almaarufu diabetes huenda ukasababisha kupotea kwa nguvu za macho au hata kukatwa viungo vya mwili kwa hivyo ni vyema mtu apate kupimwa mara kwa mara. Mwanahabari wetu carol nderi anatupasha mengi katika makala yetu ya afya yako.