Rais mwai kibaki ametoa majina ya watu tisa wanaosubiri kuidhinishwa na bunge kuchukua nafasi ya mwenyekiti na makamishna wa tume ya uchaguzi na mipaka. Isaack hassan amependekezwa kuwa mwenyekiti wa tume hiyo huku  yusuf nzibo, abdullahi sharawe, thomas letangule, mohammed alawi, lilian mahiri, muthoni wangai, albert bwire na kule galma godana wakipendekezwa kuchukua wadhifa wa makamishna wa tume hiyo.huku hayo yakijiri utata mpya umeibuka kuhusiana na kubuniwa kwa maeneo mapya 80 jinsi ilivyonakiliwa kwenye katiba mpya huku wizara ya sheria ikisema kuwa itakuwa vigumu kwa maeneo hayo kubuniwa kabla ya uchaguzi mkuu ujao.


Isaack to chair IEBC