Familia moja kutoka eneo la kisauni mjini Mombasa imefanya maandamano jijini humo ikitaka kutiwa nguvuni kwa maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Nyali. Maandamano hayo yalishinikizwa na kifo cha kijana wao ambaye alifariki katika seli za kituo hicho baada ya kutiwa nguvuni siku ya jumatano . Wazazi wa kijana huyo wanadai kuwa kijana huyo alipigwa na kujeruhiwa vibaya na maafisa wa polisi. Tukio hili linajiri wakati ambapo maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Kiambu wanadaiwa kutekeleza uovu sawia na huo uliopelekea kifo cha mwalimu mmoja wa shule ya upili ya Loreto