Kijiji cha malinda wilayani Bungoma ya magharibi, kinaomboleza vifo vya baadhi ya vijana wao walioripotiwa kuzama katika mto lwakhakha. Kulingana na ripoti ambazo hazijathibitishwa,baadhi ya vijana hao walizama baada ya kuwakwepa maafisa wa polisi waliokua wakiwaandama walipokuwa wakijaribu kuingiza bidhaa za magendo ikiwemo kahawa nchini Uganda. Hadi sasa miili ya vijana 3 imeweza kuokolewa huku vijana wengine wakiripotiwa kupotea kufikia sasa.


Mkasa Wa Lwakhakha