Huenda waliowekeza katika miradi ya ubia au pyramid schemes wakaambulia patupu baada ya benki kuu ya Kenya sasa kukana madai kuwa ilisimamisha akaunti za miradi hii na kushikilia pesa zilizotapeliwa wawekezaji.Muungano wa wawekezaji hao ulipokea barua hiyo leo hii licha ya dalili hapo awali kuonyesha kuwa hatimaye serikali ingewarejeshea fedha zao. Muungano huo sasa umeapa kufanya yote wawezalo kupata pesa zao wakiwaagiza wenzao kujiandaa kwa mgomo kuishinikiza serikali kuelezea pesa hizo ziko wapi.


Miradi Ya Pyramid