Kijiji kimoja huko Kiambu kinaendelea kuomboleza msiba ulowapata baada ya watu watano kufariki kutokana na unywaji wa vileo hatari. Huku mipango ya mazishi ikiendelea bwana mmoja aliyeponea kifo baada ya kunywa kileo hicho anaendelea kupokea matibabu katika hospitali moja eneo hilo licha ya kupofuka.