Mkamu wa Rais Kalonzo Musyoka ametoa taarifa rasmi ya serikali bungeni kuhusu afya ya waziri mkuu Raila Odinga. Hii ni kufuatia maswali ya wabunge waliotaka serikali kuelezea hali ya afya ya Waziri Mkuu, na iwapo anapokea matibabu ya kutosha nchini. Wakati huo huo mabalozi kadhaa wa kigeni walifika katika hospitali ya Nairobi kumjulia hali waziri mkuu, ambaye kwa mujibu wa daktari wake anaendelea kupata nafuu.