Rais na makamu wake hii leo walitofautiana hadharani kuhusiana na msimamo wa serikali kuhusu katiba, hii ni baada ya makamu wa rasi kusema kudai kuwa muda wa kuifanyia rasimu marekebisho bado upo. Rais kwa upande wake alisema hamna kurudi nyuma tena na msimamo wa serikali kuiunga mkono rasimu utasalia. Rais aliwataka wakenya kuikubali rasimu akisisitiza kuwa katiba haiwezi kutosheleza kikamilifu matakwa ya kila mtu. Alisema nafasi ya kuifanyia marekebisho katiba itakuwepo pindi itakapopitishwa.


Rasimu Ya Katiba