Masikitiko makuu yanazidi kuikumba sekta ya maziwa baada ya wafugaji kushindwa kupata mnunuzi. Licha ya ushauri kwa serikali kutafuta mbinu za kupunguza uharibifu wakulima katika eneo la ol-kalau walilazimika kumwaga lita elfu kumi za maziwa katika kituo kimoja cha kukusanya maziwa cha ol-kalau huko Nyahururu. Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya kampuni za maziwa kukosa kufika kuyachukua maziwa hayo kama ilivyo kawaida.  Je, serikali imekuwa kipofu kwa hali hii kwenye sekta ya kilimo? au inasubiri kufungua macho tena wakati kiangazi kitakapoingia ili iombe msaada wa chakula baada ya kutizama maziwa yakienda hasara.


Milk Crisis In Olkalau