Tuupige vita ukeketaji ili kumnasua mtoto wa kike nchini.
Ni jambo la kusikitisha kwamba katika dunia ya leo bado kuna jamii ambazo zinaendeleza tamaduni zilizopitwa na wakati. Mojawapo ya tamaduni hizo, ni swala la ukeketaji wa wanawake.
Hapa hii tabia haifai hata kutajwa katika jamii zetu,kando na kutumika!
Miezi mitatu iliopita,nilikua katika harakati za kukusanya taarifa flani ya changamoto za magonjwa yatokanayo na utapia mlo. Nilishangaa sana kukutana na wanakijiji flani sehemu ya kaskazini mashariki,wakinung’unuzana mambo ya ukeketaji. Kuna waliopinga na ndani walikuwemo walioshabikia uovu huu dhidi ya mtoto wa kike na hata mwanamke mtu mzima.
Kilichonivutia zaidi ni gumzo hilo kufanywa hadharani na watu waze,ambao ni wa kuheshimika katika jamii,lakini gumzo hilo kwa mtu aliye na ufahamu wa madhara ya ukeketaji kwa mtoto wa kike, bila shaka,lingeandamana na kulipuuza, lakini nikatega sikio makini. Maana nilipata taarifa nzuri ya kuiangazia.
READ MORE
Migori clergy condemn attack of pastors, re-circumcision of men and FGM on rescued girls
From cries and curses, how Kenyan girls are being tortured by FGM years after ban
KNCHR decries prevailing challenges amid progress in legislation
Kenyan girls still afflicted by genital mutilation years after ban
Hii si mara yangu ya kwanza kuangazia taarifa za uovu wa ukeketaji katika jamii, ila ilikua mara ya kwanza kupata kuisikia kutoka kwa jamii ya Kaskazini mashariki. Kwamba wao wameitumia tamaduni hii kuwadhalilisha watoto wao wa kike,ilikua ni jambo la kunishangaza miongoni mwa jamii ambayo imejikita mizizi na ucha Mungu,yaani kwenye misingi ya dini ya kiislamu.
Niliwahi kushuhudia maadhimisho mbalimbali ya kupinga ukeketaji na kukaribisha tohara mbadala. Sana nimejonea miongoni mwa jamii ya Wamasai. Ni tamaduni iliokita mizizi sana lakini katika jamii yao,lakini kuna jitihada kutoka kwa mashirika ya kijamii,kwa ushirikiano na serikali kupinga ukeketaji wa mtoto wa Kike.
Kupitia utafiti wa serikali na hata shirika la UNICEF, matokeo yao yanaashiria kuna mbinu za kisasa za ukeketaji,ambzo unakuta mtoto mdogo tuseme wa umri wa miaka 3-5 hukeketwa na mapema. Kisha kwenye matokeo yayo hayo pia waligundua kuna maafisa wa matibabu wanaotumiwa kutekeleza tohara ya kina dada,nadhani hatua zitachukuliwa hapa aisee..
Kwa nini nazungumzia swala la ukeketaji? Lipo na linaendelea katika jamii tunamoishi. Unapoona familia inamsafirisha mtot wa kike kutoka ughaibuni wanakoishi,hadi nchini Kenya kukeketwa,jamani, dunia imeisha. Kwani huu ndio uozo unafaa tuupinge kwa namna yeyote ile na kumlinda msichana na haki za viwiliwili vyake kutoka utosi hadi nyayo.
Ukeketaji una madhara tofauti kwa mtoto wa kike. Madhara ambayo nitayaangazia zaidi ni ile kumharibu tupu ya mtoto kisha anapata matatizo wakati anapokuwa mkubwa na anataka kuzaa. Inakua vigumu kiasi kwa kujifungua salama na vyema.
Athari za usalama wa mtoto na mamake ni sawa na kuekwa kwenye mizani ya uhai. Ni aidha mmoja afe mwengine aishi, wote wake au wote waishi. Na inapofikia hapa,basi ni sawa na kumkatia mtu maisha ya baadae pale jamii inapofikiria kumkeketa.
Mashara mingine ni kama kumnyima haki mtoto wa kike ya viwiliwili vyake, ndoa za mapema, kumkatiza ari ya kusoma maishani wakati siku za usoni hatokua na imani na uajibikaji wa majukumu yake maishani.
Jamani tuipinge hii tohara ya wasichana na wanawake katika jamii tunamoishi.Unapoona matokeo yakiashiria upungufu wa asilimia 21, basi tujizatiti na kuendelea kupinga uovu huu katika karne ya leo. Wazazi hawafai kamwe kuwapeleka watoto wao kukeketwa. Mtoto ana haki ya kuheshimiwa viwiliwili vyake pasi kusukumwa,iwe wajibu.
Ali Manzu ni mtangazaji na mwanahabari wa @KTNLeo wasiliana naye kupitia mitandao ya Kijamiiya twita @Ali_Manzu na pia Facebook Ali Manzu. Pia unaweza kumuandikia kupitia barua pepe manzuali@gmail.com