Na Carren Omae
Katika hatua ya kutafuta uungwaji mkono kutoka maeneo yote nchini, Chama cha Labour Party of Kenya LPK kinatarajiwa kuendeleza ziara katika maeneo mbalimbali ya Pwani. Kwenye taarifa, Katibu Mkuu wa chama hicho, David Makali amesema ziara hiyo inatarajiwa kuanza wikendi hii.
Wakiongozwa na kiongozi wa chama hicho ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa chama cha ODM, Ababu Namwamba, viongozi hao wanatarajiwa kuzuru eneo la Mombasa kuanzia kesho kisha Kaunti ya Kilifii. Kulingana na Namwamba chama hicho kinatarajiwa kufungua ofisi zake eneo la Kwale ambapo pia watatangaza wagombezi wa viti mbalimbali kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.
Chama hicho kilianza kampeni zake wiki iliyopita kwa kuzuru maeneo ya Bungoma, Busia na Kisii ambapo vilevile kilifungua ofisi zake.
Baada ya ziara ya Pwani LPK inayatembelea maeneo ya Bonde le Ufa katika Kaunti za Uasin Gishu, Elgeyo Marakwet na Kajiado.?
READ MORE
History will repeat itself if the Opposition goes to 2027 elections divided
Missing political supremo, the vacuum disturbing ODM
'Sisi ndio Sifuna': Why the dynamic duo must find ways to sustain wave