Siku tatu baada ya kifo cha aliyekuwa waziri wa mazingira, John Michuki- Kenya inaomboleza tena. James Njenga Karume, mwanasiasa mkongwe amefariki leo asubuhi. Karume alifariki katika hospitali ya karen hapa Nairobi. Karume alikuwa anaugua saratani kwa muda mrefu, ingawa familia yake imesema amefariki kutokana na homa ya mapafu ama pneumonia. Karume alikuwa na miaka 83. Viongozi kadhaa akiwemo rais Mwai Kibaki, mwandani mkuu wa karume wametuma rambi rambi zao.