Washikadau katika sekta ya matatu wanaendelea kupinga vikali azma ya serikali kuziondoa barabarani matatu za abiria 14 huku wakiapa kuchukua hatua za kisheria endapo wizara ya uchukuzi haitabadili sera hiyo.naibu mwenyekiti wa muungano wa maslahi ya wenye matatu nchini john katimbwa amesema hatua hiyo itawaongezea wadai hao gharama mbali na kuwakosesha ajira wakenya laki tano .