Huku serikali ikitangaza mipango ya kuwashawishi wakenya kuanza kuhusika katika upangaji wa uzazi,mzee mmoja mwenye umri wa miaka 80, kutoka kaunti ya Kilifi anasema kwamba huko ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa,kwani ni kwake yeye hilo ni jambo lisilowezekana. Mzee Shutu Mwango anajivunia kuwa na wake 5,watoto 40 kando na wajukuu na vitukuu, ali manzu alikutana na mzee huyo ambaye wake zake ndio wanaokwenda mbio katika kutekeleza majukumu ya familia yake huko Tezo, Kilifi.