Imetimia miaka thelathini tangu kutambulika kwa virusi vya ukimwi kwote ulimwenguni. Jee kumekuwepo na mabadiliko yeyote? Au maambukizi ya virusi vya ukimwi yamezidi kuongezeka? Waziri wa jinsia Esther Murugi amesema kuwa miradi kadhaa kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikali imeweza kuchangia katika kupunguza maambukizi ya virusi na wengi ya wanaoishi na virusi vya ukimwi kwa sasa wanaweza kuishi miaka mingi baada ya uvumbuzi wa dawa za arv. Taarifa ifuatayo inamulikachangamoto za vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na mwelekeo unaopasawa kufuatwa katika kampeini hiyo?