Wenyeji wa kijiji cha mundere katika kaunti ya busia, bado wanashangazwa na uwepo wa nyoka mweupe aliyejipinda katika mojawapo ya nyumba kijijini humo. Huku akiaminika kuwa tu nyoka wa kawaida aliyepotea njia na kuingia nyumbani humo, wazee wa kijiji hicho wanadai kwamba nyoka huyo ni mizimu ya kale na anahusishwa na kurejea kwa mke wa marehemu wa kijana wa boma husika.  Ni kisa kinachogonganisha imani ya itikadi za kale na mwelekeo wa kisiasa.


snake;busia;