Kiongozi wa mashataka katika mahakama ya ICC Louis Moreno Ocampo ametangaza kuwa hana nia yoyote ile ya kuwatumia mashahidi walioibuka wakidai kuhongwa ili kutoa ushahidi wa urongo. Ujumbe kutoka afisi ya Ocampo umekariri kuwa mashahidi hao hawakutoa ushahidi mbele ya afisi hiyo, na kuwa kabla ya kuwatumia mashahidi wowote wale afisi hiyo hufanya uchunguzi wa kina kuhusu shahidi yeyote yule. Vile vile Ocampo ametangaza kuwa ana habari za watu ambao wanajaribu kuwahonga au kutisha mashahidi.


Ocampo Kuhusu Mashahidi