Kufikia sasa, timu za Gor mahia na Ulinzi stars bado ziko na nafasi ya kutwaa taji la ligi ya kandanda msimu huu.Ulinzi watanyakuwa taji hilo iwapo watashinda dhidi ya karuturi sports siku ya jumapili katika uwanja wa afraha iwapo tu Gor mahia watapoteza mechi yao dhidi ya city stars. Ni alama moja tu inayotenganisha timu hizi mbili. Mechi kati ya Gor mahia na City stars huenda itachezwa katika uga wa Nyayo au City stadium.


Kipindi Cha Lala Salama