Huku wizara ya mipango ikitarajiwa kutangaza rasmi matokeo ya hesabu ya kitaifa ya watu iliyofanywa mwaka jana wakenya wanajiuliza maswali mengi kuhusu sababu za kucheleweshwa kwa matokeo hayo, huku uvumi mwingi ukichipuka. Je ni yepi yaliyosababisha matokeo hayo kukawia? ni kwa nini hadi leo baadhi ya makarani na maafisa waliofanya kazi ya sensa hawajalipwa pesa zao?